Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kipindi cha televisheni “Upeo wa Ushindi; Mwisho wa Dola ya Marekani na Kuibuka kwa Mpangilio Mpya wa Dunia” kilifanyika siku ya Jumatatu tarehe 4 May kwa juhudi za Majma’ ya Kimataifa ya Qadimun, na kwa ushiriki wa kundi la shakhsia za kidini na kisiasa kutoka nchi mbalimbali, na kilirushwa kupitia vituo vya Al-Kawthar na Safir.
Muhammad Zaman Zamani, Imamu wa Swala ya Ijumaa miongoni mwa miji ya kusini mwa mkoa wa Fars, katika hotuba yake huku akirejelea sunna za Mwenyezi Mungu katika historia alisema: Kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’ani, kila nguvu inayopatwa na uasi, dhulma na ufisadi, hatimaye hukabiliwa na kudhoofika na kuporomoka, na kanuni hii imekuwa ni ya kweli kwa nguvu zote katika historia.
Akiashiria mabadiliko ya kisasa aliongeza kuwa: Marekani pia haiko nje ya kanuni hii, na utendaji wake katika miongo ya hivi karibuni, hasa katika uhusiano wake na nchi mbalimbali, umepelekea kujitokeza kwa changamoto kubwa kwa taifa hilo.
Imamu huyo wa Swala ya Ijumaa huku akirejelea maendeleo ya hivi karibuni katika uwanja wa kijeshi alisema: Matukio ya karibuni yameonesha kwamba; ubora wa kijeshi peke yake si dhamana ya kudumu ya nguvu, na mizani inaweza kubadilika.
Zamani pia aligusia vipengele vya kisiasa na kiuchumi vya suala hili na akasisitiza: Katika nyanja ya kisiasa, baadhi ya maamuzi na mielekeo imekabiliwa na ukosoaji mpana, na katika uwanja wa kiuchumi pia kuna changamoto ambazo zimeathiri nafasi ya nchi hiyo katika kiwango cha kimataifa.
Akaongeza kwa kusisitiza kwamba; nguvu halisi iko katika uadilifu, uhalali na mwenendo unaojengwa juu ya misingi ya kibinadamu, na akabainisha: Kila mara misingi hii inapodhoofishwa, mazingira ya kupungua kwa ushawishi na hadhi hujitokeza.
Mwishoni, mwanachuoni huyu wa Kisunni akielezea matumaini yake kuhusu mustakabali, alisisitiza: Mabadiliko yanayoendelea yanaweza kuwa msingi wa mabadiliko muhimu katika muundo wa nguvu za dunia, na ni lazima mchakato huu ufuatiliwe kwa umakini na uangalifu.
Maoni yako